Ruto amjibu Kabogo kuhusu kampeni za mapema

President Uhuru Kenyatta with Deputy President William Ruto at the late De' Mathew's funeral service in Murang'a
President Uhuru Kenyatta with Deputy President William Ruto at the late De' Mathew's funeral service in Murang'a

Naibu rais William Routo amepuuzilia mbali madai kuwa anajihusisha sana na siasa za mwaka 2022 badala ya kuangazia ajenda ya maendeleo.

Ruto, ambaye anajulikana kwa vichekesho vyake katika mikutano ya hadhara, hakuchelea kuchangamsha waombolezaji katika mazishi ya De Mathew.

Alikuwa akijibu matamshi ya aliyekuwa gavana wa Kiambu William Kabogo aliyesema kwamba Ruto anapendwa na watu lakini anafaa kuacha kampeni za mwaka 2022.

"Rais, Kabogo saa zingine ni mchokozi kwa sababu amekuja kunishtaki kwako ati huwa napenda kufanya siasa... Hiyo maneno si ukweli," Ruto alisema.

Kabogo alikuwa amemuambia rais Uhuru Kenyatta kuwa Ruto alikuwa miongoni mwa watu wawili waliokuwa wanafanya kampeni za mwaka 2022.

"Mheshimiwa Rais Kuna watu wawili Wana uwezo ya kutuliza mambo ya 22. Mmoja ako hapa mwingine nilimualika na hajafika. Wote ni marafiki zangu. Deputy President, watu wanakupenda but tufanye kazi kwanza," Kabogo alisema.

Ruto alisema kwamba watu wanamshambulia bila sababu na kusahau kwamba aliapishwa kuwa naibu wa rais wa Kenya.

"The problem is these people forget and put me in the same class with people who don't have any responsibilities and duties. My friend I was sworn in and assigned duties to help President Uhuru Kenyatta," Ruto alisema.