Kriss Darlin aelezea sababu ya kumpigia Raila Odinga magoti

kriss darlin
kriss darlin
Siku moja baada ya kanda ya DJ Kris Darlin akimpigia Raila Magoti kuenezwa kote, msanii huyo amejitokeza kutoa sababu alifanya hivyo.

Hii ni baada ya wananchi kutoka tabaka mbalimbali kujitokeza na kumkashifu kwa tendo hilo.

Katika kanda ile, Darlin anaonekana akimwambia kiongozi wa upinzani, Raila Odinga,

“Nimeskia kuwa kuna vijana wengi bungeni ambao wanapigana na baba (Raila), nikubalishe kama kijana mwenzao kupigana nao humo ndani huku ukingoja kupigana mwaka wa 2022," alisema Darling huku akiwa amepiga magoti mbele ya Raila.

Isitoshe Darlin alisema yupo tayari kupigwa risasi kwa niaba ya kiongozi huyo wa ODM kama hiyo ndio itamfanya aongoze nchi mwaka wa 2022.

“Wacha wanipige risasi, kama itamaanisha utaongoza 2022....Naomba unishike mkono Baba.." Aliendelea huku umati ukishangilia.

Katika mahojiano ya simu na gazeti la The Star, DJ huyo alisema kuwa hakuwa anatafuta umaarufu alipompigia Raila Odinga magoti.

"Raila amekuwa mbunge wa eneo hilo kwa zaidi ya miongo miwili na kwa sababu Kibra ni eneo la ODM jijini Nairobi, yeye ndiye atakuwa na tamko la mwisho la ni nani atakayemrithi Okoth," Alisema.

Hata hivyo, alisema uamuzi wa atakaye chaguliwa kama mbunge wa Kibra upo na wananchi wa Kibra na sio Raila pekee.

"Watu wa Kibra ndio wana uamuzi wa mwisho. Nikichaguliwa nitawakilisha chama cha ODM, sio Raila," Aliongeza.

Darlin anaamini kuwa yeye ndiye mgombea anayefaa kwani alizaliwa na kulelewa Kibra na kuwa anaelewa vyema masaibu yanayokumba mtaa huo wa madongoporomoka.

Aliongeza akisema kuwa amekuwa akifanya miradi ya kusaidia wananchi Kibra.

"Mimi hutoa taulo za hethi kwa shule za wasichana wa Kibra, pia huwa natoa suruali za ndani kwa vijana. Nina shindano la kadanda liitwalo Kriss Darling Supercup ambalo limekuwa kwa miaka minne sasa," Alisema.

Darlin on August 21 presented his official documents to the ODM headquarters.