Machifu wakamatwa Wajir wakiongeza idadi ya watu katika Sensa

CENSUS
CENSUS
#WajirCensusFraud ilitamba kwenye twitter siku ya Jumanne baada ya wakenya kulalamikia kuhusu uhalali wa zoezi linaloendelea la kuhesabu watu.

Wakenya katika twitter walitilia shaka zoezi zima la kuhesabu watu baada ya afisa mmoja wa kuhesabu watu kupatikana amesajili watu 600 badala ya idadi iliolengwa ya watu 100. Hii wanaamini ni njama ya wanasiasa kuongeza idadi ya watu katika maeneo wanamotoka kwa manufaa ya kisiasa, hasa katika maeneo yenye watu wachache na wanao kaa mbali mbali.

Hii inajiri siku moja baada ya machifu wawili na naibu wa chifu katika eneo la Wajir kutiwa mbaroni kuhusiana na ulaghai katika zoezi la kuhesabu watu

"Those altering the numbers in Wajir East, Eldas and Tarbaj are after own political interests,"@bosiboriviews alisema.

@kiilundeti aliuliza, "The question is, can we ever get anything right as Kenyans?"

Akithibitisha kukamatwa kwa machihfu hao, kamishna wa kaunti ya Wajir Lyford Kibaara alisema walihusika katika kuongeza idadi ya watu katika lokesheni zao.