Tanzia! Aliyekuwa mwenyekiti wa TLB Hassan Kamwaro aaga dunia

KAMWARO
KAMWARO
Aliyekuwa mwenyekiti wa bodi la Leseni za uchukuzi nchini TLB Hassan Ole Kamwaro ameaga dunia.

Kamwaro amekuwa akiugua saratani, na alifariki akipokea matibabu katika Mercy Hospital,mjini Oklahoma Marekani.

Kamwaro amekuwa akiugua saratani ya umio (koo) na alikuwa amesafiri Amerika kwa matababu zaidi. Mwanawe Jedida Kamwaro alithibitisha kifo chake siku ya Jumatano. Mwaka 2010, aliyekuwa rais Mwai Kibaki alifutilia mbali uteuzi wa Wilfred Lengei na kisha kumtaja Kamwaro kama mwenyekiti wa TLB.

Mwaka 2012, Kibaki alimteua Mhandisi Joseph Kamau kusimamia bodi ya TLB kuchukuwa nafasi ya Kamwaro.

Kamwaro alimuoa Eunice Sission mwaka 2012 katika hafla ya kibinansi iliyohudhuriwa na viongozi wa eneo analotoka pekee yao.