Rayvanny ashtumiwa kutoka kimapenzi na Lulu. Dogo kafuata nyayo za Diamond Platnumz

Kwa kile kinachoonekana kama Dogo Rayvanny kufuata nyayo za mkurugenzi wa lebo ya Wasafi na staa mkubwa barani Afrika Diamond Platnumz, taarifa kitaani zinakwenda kuwa huenda dogo anachepuka kimapenzi na muigizaji ambaye aliwahi kuhukumiwa kosa la mauaji.

Jisomee hadithi hapa:

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Elizabeth “Lulu” Michaels anaonekana katika matukio zaidi ya moja akiwa katika hali tatanishi na staa huyu wa Tetema taarifa na ambazo baby mama wa Rayvanny  Fahyma amezikana.

Pata uhondo kamili:

Wanasema kuwa mapenzi ni kama kikohozi hayafichiki. Iwapo kweli staa huyu anachepuka na kusaliti penzi la baby mama litakuja kujiweka wazi. Rayvanny anatamba na mkwaju wa Tetema ambao ulipata kufungiwa kuchezwa katika vyombo ya habari nchini.