RED CARD?Mbona Mariga Huenda akazuiwa kuwania kiti cha Kibra .

MCDonald Mariga
MCDonald Mariga
Kwa Mukhtasari

  • Washirika wa Ruto waliunda  undi la kumkochi Mariga kuhusu maswali yote ambaye angeulizwa wakati wa kuhojiwa na bodi ya  uchaguzi .
  • kati ya wanachama sita wa bodi ya uchaguzi ,Watatu ni washirika wa karibu wa Ruto .

Mchezaji wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya Kenya Mcdonald Mariga  huenda akazuiwa kuwania kiti cha eneo bunge la Kibra  katika uchaguzi mdogo wa Novemba tarehe  7. Imefichuliwa kwamba Mariga anapendekezwa na  Naibu wa Rais William Ruto kinyume na matakwa ya baadhi ya viongozi wa chamna cha Jubilee . Mmoja ya wagombeaji  waliotaka kupewa tiketi ya Jubilee katika uchaguzi huo siku ya jumanne aliwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa Kumpa Mariga tiketi hiyo  akisema ilifanywa kwa njia isiofaa,wongo na iliyoghubikwa na usiri mkubwa .katika rufaa yake Morris Peter Kinyanjui   pia ameashiria kwamba  kwamba Mariga   hajasajiliwa kuwa mpiga kura .

“ Ili kufanya mambo kuwa hata mabaya zaidi ,mtu aliteyeuliwa si mkaazi wa kibra  na kuna shauku kubwa iwapo amewahi kupiga kura’ Kinyanjui amelalama ." mgombeaji huyu atakuwa kazi ngumu kumwuuza kibra  ikilinganishwa na hadhi ya mtangulizi wake’ . Katibu wa mkuu wa chama hicho Raphael Tuju  amelithibitishia gazeti la The Star kwamba rufaa hiyo imewasilishwa na mlalamihsi mmoja ." Kilichofanyika hivi punde sasa kinamaanisha kwamba lazima tuiarifu IEBC kuhusu ugombeaji wa Mariga  huku bodi  ya rufaa ikishughulikia suala hili’ amesema Tuju .

Duru zaarifu kwamba Mariga alisajiliwa kama mpiga kura katika eneo la  Karioakor wiki mbili zilizopita na huenda asizingatiwe kama mpiga kura nchini  katika kipindi cha muda mfupi ujao . Hii ni kwa sababu orodha   ya hivi punde  ya  wapiga kura haijawekwa katika gazeti rasmi la serikali kama inavyohitajika na sharia . Mara  ya mwisho Chebukati alipoiweka katika gazeti rasmi la serikali sajili hiyo ilikuwa mwaka wa 2017 . Lakini mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya chama cha Jubilee  Andrew Musangi amekuwa mwepesei wa kupuuza madai hayo kama uvumi akisema alichohitaji ni  kusajiliwa kama mpiga kura .