logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tobiko hacheki na mtu hata samaki wakubwa watavuliwa Mau

Tobiko hacheki na mtu hata samaki wakubwa watavuliwa Mau

image
na

Habari02 October 2020 - 03:14
TOBIKO
Serikali imeeleza bayana kwamba haitasaza mtu yeyote aliyenyakua ardhi kwenye chemichimi za maji kote lnchini.

Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko siku ya Jumanne alieleza kwamba awamu ya pili ya kufurusha watu kutoka Msitu wa Mau italenga pia watu mashuhuri walionyakuwa ardhi katika msitu huo.

"Hakuna mtu atakayetumiwa kama kafara," alihakikishia kamati ya bunge ya mazingira.

Alikuwa akijibu maswali ya mwenyekiti wa kamati hiyo Kareke Mbiuki aliyetilia shaka zoezi hilo," tuna ugumu kwa sababu unalenga tu wananchi wa kawaida na ilhali ni wazi ni akina nani wanamiliki ardhi ndani ya misitu. Wanafaa kuwa wa kwanza kufurushwa." Mbiuki aliahidi waziri Tobiko kuwa wakenya watamuunga mkono ikiwa atawakabili “samaki wakubwa”.

Wabunge walimuita Tobiko ili aeleze bayana kuhusu awamu ya pili ya kuondoa watu kutoka msitu wa Mau.

"Nitawapa ilani {wale wote katika msitu} lakini nataka hakikisho kutoka kwa kamati hii kuwa itaunga mkono mpango huu," alisema. Anahitaji raslimali na maafisa zaidi.

Rais Mustaafu Daniel Moi ni miongoni mwa watu mashuhuri waliotajwa na kamati hiyo kumiliki ardhi ndani ya msitu wa Mau.

 .

Moi anamiliki kampuni ya majani chai ya Kiptagich inayomiliki jumla ya ekari za ardhi 2,223.945.

Naibu mwenyekiti wa kamati hiyo Sophia Abdi na wanachama Beatrice Kones (Bomet), Hulufo Hassan (Isiolo North), Benjamin Washiali (Mumias East) na Hillary Kosgei (Kipkelion West) walihudhuria kikao hicho.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved