Mjomba wangu alikua ananyonyesha mtoto sehemu za siri - Gladys

Kwa kweli kuna watu na viatu duniani.

Juzi mwanadada kwa jina Gladys aliyejawa na ujasiri alimuanika mjombake, miaka mingi baada yake kutenda unyama ulio angamiza mwanawe.

Kulingana na mwanadada huyu, akiwa mdogo alikuwa anaishi kwa shangazi yake na pindi tu alipojifungua alishuhudia tendo ambalo mpaka wa leo humsumbua akili.

Akizungumza na Massawe Japanni alisema kuwa shangaziye akienda kazini, mjombake alikuwa anamnyonyesha mtoto sehemu zake za siri kila anapolia.

Anasema alipopiga ripoti kwa shangaziye,  mjombake alijitetea akisema kuwa hafai kumuamini Gladys kwani alikuwa mtoto na akili za kitoto tu.

Mjombake aliendelea na tendo lile na siku mmoja mtoto akapata maambukizi ya kifua ambayo yalipelekea kifo chake. Walipofuatilia jambo hilo, mjomba yule alikuwa tayari ametoweka asijulikane alipo.

Soma usimulizi wake Gladys.

Mimi nilikuwa nakaa na auntie yangu but sasa nilikuwa kitu 10 years, na sasa huyo auntie alikuwa anaenda kazi na mzee wale watu wa biashara alikuwa anabaki nyumbani.

Sasa auntie alikuwa amejifungua na hawezi kaa na mtoto ile mimi pia naenda shule, sasa kitu kama weekend tukiwa pale yaani alikuwa anafanyia ule mtoto maajabu akisema huyo sio mtoto wake.

Mtoto akilia anaanza kumnyonyesha sehemu zake za siri imagine. Sasa mimi nikiambia auntie huyo bwana anamuambia ni ni akili za mtoto tu, eti hawezi fanya kitu kama hicho.

Mpaka mtoto akaoza kifua akawa sasa ni kesi ingine na ikawa too late, hiyo kitu ilini affect sana. Yaani huyo mtoto wamezaa naye lakini anasema kwa sababu auntie anaenda kazini mimba sio yake.

Baadaye ilipokuja julikana alikuwa hajulikani aliko.