Nyota Mariga kufahamu Jumatatu iwapo atawania kiti cha Kibra

Nyota wa soka McDonald Mariga kesho atafahamu iwapo atawania kiti cha eneo bunge la kibra.

Kamati ya kusuluhisha mizozo ya IEBC kesho alasiri itatoa uamuzi wa iwapo mariga alisajiliwa ifaavyo kama mpiga kura ili aruhusiwe kuwa katika kinyanganyiro hicho novemba tarehe 7.

Hayo yakijiri, timu ya Kenya ya voliboli ilishindwa mchuano wao wa pili katika kampeini yao ya kombe la dunia huko Japan baada ya kuzabwa seti tatu kwa nunge na uholanzi mapema hivi leo.

Hata hivyo Malkia strikers chini ya ukufunzi wa Paul Bitok walionyesha mchezo ulioboreka dhidi ya uholanzi ikilinganishwa na walivocheza na marekani jana.

Warembo hao wa Kenya wana muda mfupi wa kurejea ulingoni kwa kishindo kwani kesho aubuhi watachuana na Serbia katika mchuano wao wa tatu.

Waakilishi wengine wa Afrika katika mashindano hayo Cameroon walishindwa pia seti tatu kwa nunge dhidi ya Uchina  baada ya kuzabwa jana seti tatu kwa nunge na urusi.

Katika soka kocha wa kilabu ya Bandari Bernard Mwalala amesema alifurahishwa na ushindi wa mabao mawili kwa nunge wa vijana wake dhidi ya kilabu ya Tunisia  US Ben Guerdane  I kwenye mchuano wa kombe la caf confederation hapo jana  lakini amesema bado wana kibarua cha kutetea ushindi huo katika mkondo wa pili  jijini Tunis wiki mbili zijazo .