PATANISHO: Mume wangu alizaa na rafiki yangu

Bwana Nahashon aliomba apatanishwe na mkewe bi joyline akisema kuwa walikosana na mkewe na akaondoka huku akimuachia watoto.

Mke wangu ilifika mahali akaanza kuwa rude, akaanza kubishana nami na hata maji hakuwa ananipelekea bafuni. Hapo tukabishana na nikampa fursa akapumzike nyumbani.

Katika harakati Ile nilipata mwanadada mwingine lakini alikuwa anatesa watoto wangu na pia Hana usafi lakini tulitengana.

Nahashon anasema heri mke wa Kwanza ambaye wametoka mbali na ambaye anapenda kuliko mwanamke mwingine.

Alipopigiwa simu bi Joyline alikata simu pindi tu aliposkia yupo hewani, mara ya pili alisema kuwa kamwe hataki kuongea na mumewe.

"Sasa sijui nitasemaje labda ameogopa na yeye huogopa kuongea na watu. Hawa watoto bado ni wake na kuna vile vitu wanaweza kosa kutoka kwa mama mzazi." Alisema Nahashon.

Joyline alisema,

"Siwezi rudi sahizi kwani hawezi badilisha tabia na umuulize huyu ni mke wa ngapi? Leo huwa mzuri kesho anabadilika na mipango zake za kando ndio zilifanya nibadilike."

Aliongeza, nilikuwa na rafiki baadaye alimchukua akamleta kwa nyumba yangu, akanifukuza na wakabaki naye. Isitoshe alizaa na rafiki yangu." Alipopewa fursa ya kujitetea, Nahashon alisisitiza kuwa mwanadada huyo sio rafiki yake na mtoto huyo sio wake kwani vipimo vya DNA vilithibitisha.