Habari zote Muhimu Leo Jumanne 15/10/2019

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
  

Mabunge ya  Kaunti za Kisumu  na tana river  yameukataa mswada wa punguza mizigo . huko kisumu waakilishi wa kaunti waliukataa mswada huo baada ya mjadala wa saa moja wakisema kwamba unatishia kuhujumu  katiba mpya iliyopitishwa mwaka wa 2010.katika bunge la kaunti ya tana river ,waakilishi wa kaunti wamesema kupunguza uakilishi sio jambo litakalowasaidia wakaazi wa eneo hilo.

Sarah Wairimu mjane wa  Tob  Cohen  amewasilisha  kesi kortini  akitaka mkurugenzi wa DCI na  DPP kuchukuliwa hatua kwa kukaidi agizo la mahakama .wairimu kupitia wakili wake Philip Murgor  amesema wawili hao wamekiuka agizo lililotolewa na jaji Jessie Lessit  kuwazuia kuzungumza na wanahabari kuhusu  kesi ya mauaji ya mumewe .

Inspekta  mkuu wa polisi Hillary Mutyambai ameagizwa kuanzisha uchunguzi  kuhusu madai ya   vitendo vinavyokiuka sheria na uhalifu  katika idara ya uhamiaji . Hii ni baada ya ufichuzi uliotolewa katika runinga ya Citizen  kuhusu njama ya maafisa wa polisi na wale kutoka idara hiyo kutumia vitisho  vya kumfurusha nchini mfanyibiasha mmoja wa asili ya kiasia ili kuichukua mali yake . msemaji wa wizara ya usalama wa ndani Wangui Muchiri amesema  Mutyambai anatakiwa kuwasilisha ripoti ya  hali ya uchunguzi wake ndani ya kipindi cha siku 14 .

Mbunge wa Tiaty William Kamket  amewashtumu polisi kwa kutochukua hatua za kumtafuta mwanafunzi wa chuo kikuu aliyetekwa nyara katika kituo cha kawi ya mvuke cha olkaria ambapo alikuwa akifanya masomo ya kujifunza kazi . Kamket amesema mwanafunzi huyo alitoweka jana usiku  mjini Naivasha wakati alipokuwa akiburudika na wenzake na amemshtumu OCPD WA eneo hilo kwa kujikokota katika jitihada za kuwakamata washukiwa .

Upo katika hatari ya kuhusika katika ajali ya barabarani siku za ijumaa ,jumamosi na jumapili kuliko siku yoyote ya wiki .Takwimu za NTSA ZAONYESHA KWAMBA  watu zaidi ya 400  waliaga dunia katika ajali zilizotokea katika siku hizo  kati ya januri na oktoba . watu 500 waliaga dunia siku za jumapili ,480 siku ya jumamosi ilhali 406 waliaga dunia siku za ijumaa .

Shirika la feri  limeikabidhi familia ya  marehemu Mariam Kighenda shilingi laki mbili  ili kuisaidia familia yake kwa  matayarisho ya maazishi yake na bintiye Amanda Mutheu  . mumewe Mariam , JoHN WAMBUA PIA amepokea hundi ya shilingi elfu 682,500 kutoka kwa kampuni ya bima  kwa gari lao lilitumbukia baharini  na familia yake

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amewaomba waajiri kuwaruhusu wafanyikazi wao wanaoishi Kibra  kushiriki uchaguzi wa Novemba tarehe saba .Mudavadi amesema  wenyeji wana wajibu wa kumchagua kiongozi ataayekamilisha kazi nzuri iliyoanzishwa na marehemu Ken Okoth .

Mzozo  kati ya serikali na madreva wa magari ya mizigo unaendelea licha ya serikali kusema kwamba iliondoa agizo lililohitaji mizgo yote kusafirishwa kwa  reli ya SGR .mfanyibiashara salim karama amesema hakuna kampuni ya uchukuzi iliyorejelea oparesheni zake .

Watu 400 zaidi wamefariki katika ajali za barabarani mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana katika kipindi  sawa na hiki .takwimu za  NTSA  zaonyesha kwamba watu 2700  waliaga dunia kutokana na ajali za barabarani kufikia  mwisho wa siku jana ikilinganishwa na watu 2300 waliofariki mwaka uliopita

  Uteuzi wa mbunge wa zamani wa Othaya Mary wambui kama mwenyekiti  maamlaka ya ajira umezua lalama  kali sana mtandaoni kutoka kwa wakenya na hasa katika ukumbi wa twitter .wengi wamehoji nia ya serikali kumpa wambui kazi hiyo kwani   suala la ajira linazua hisia kutoka kwa vijana wengi nchini ambao wamezua shauku iwapo wambui  ana uwezo wa kutoa na kutekeleza sera na mikakati bunifu ya kuwawezesha vijana kupata kazi .waziri wa leba Ukur Yattani alitangaza uteuzi wa wambui katika maamlaka hiyi kupitia arifa maalum ya gazeti rasmi la serikali hapo jana .

Mwanamikakati wa mawasiliano ya kidijitali Dennis Itumbi na shahidi Samuel gateri wameshtakiwa upya kuhusiana na barua feki iliyodai kuwepo njama ya kumwua naibu wa rais William Ruto . wawili hao wamefikishwa kortini leo baada ya upande wa mashtaka kuziunganisha kesi zao . wamekanusha  mashtaka ya kuchapisha  taarifa ya wongo kinyume cha sheria .

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma  amewasilisha kesi ya ukiukaji wa agizo la mahakama dhidi ya mjane wa TOB COHEN SARAH WAIRIMU NA wakili wake Philip Murgor . DPP anasema wawili hao wanafaa kuchukuliwa hatua kwa kuzungumzia mauaji ya COHEN wakati wa maazishi yake .

Afisi ya mratibu wa bajeti imekashifiwa leo na maseneta  kuhusu kutolewa kwa pesa kwa njia isiofaa kwa ununuzi wa vifaa vya  matibabu katika hospitali za umma . aliyejipata pabaya ni kaimu mratibu wa bajeti Stephen Masha .

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yanatarajiwa kukumba  maeneo ya pwani na  kati kuanzia alhamisi wiki hii .hata hivyo  nairobi itakuwa na  vipindi vya  jua na mawingu kuanzia kesjo huku manyunyu ya mvua yakitarajiwa katika baadhi ya maeneo .huyu hapa bernad chanzu kutoka idara ya utabiri wa hali ya  anga .

Zaidi ya  hekari 1800 za mashamba yaliokuwa yamenyakuliwa yamerejeshwa kwa  serikali  katika eneo la Delamere huko Naivasha . afisa mkuu wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi twalib Mbarak amesema  hilo limeafikiwa baada ya makubaliano ya nje ya mahakama na waliokuwa wameyanyakua mashamba hayo .

Vifo vya abiria bado vipo juu  katika barabara zetu  .takwimu za NTSA  Zinaonyesha kwamba  watu 1,050  waliaga dunia kufikia mwezi huu ikilinganishwa na 900 waliofariki mwaka jana kipindi kama hicho.

Waandamanaji wanaopinga  SGR huko Mombasa wametahadharishwa dhidi ya kuvuruga sherehe za mashujaa .kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo  amesema mkutano wowote  unaopangwa kufanywa katika uwanja wa tononoka siku  ya mashujaa hautakubaliwa .

Madreva wa magari ya kibinafsi bado ndio  hatari katika baraara zetu .takwimu  kutoka NTSA  zinaonyesha kwamba  magari ya kibinafsi yalisababisha vifo vya watu 722 kati ya januari na oktoba mwaka huu  ikilinganishwa na watu 630 waliouawa na magari ya kibiashara . madreva wa matatu walisababisha vifo vya watu 415 ikilinganishwa na watu 433  mwaka jana .Emmanuel Nabiswa anaripoti .

Bunge la kaunti ya meru leo linajadili mswada wa punguza mizigo .mswada huo hadi kufikia sasa umekataliwa na kaunti 16  na ni uasin Gishu pekee ndio iliyoupitisha .

Rais wa zamani wa afrika kusini Jacob Zuma  atakata  rufaa  katika kesi ya ufisadi dhidi yake   baada ya mahakama wiki jana kutupilia mbali ombi lake kwamba kesi hiyo ifutiliwe mbali . Madai ya ufisadi dhidi ya Zuma ni  ya miaka ya 90 wakati taifa hilo lilipotoa kandarasi ya ununuzi wa sulaha .Hilo linajiri  baada ya marekani wiki jana kuiwekea vikwazo familia ya Gupta  na mshirika wao mmoja kwa tuhuma za ufisadi nchini afrika kusini . Familia ya Gupta ilikuwa na uhusiano wa karibu na Zuma na utawala wake.