Inspekta Generali aanza uchunguzi wake katika idara ya uhamiaji

ig
ig
Inspekta Generali wa polisi Hillary Mutyambai ameelekezwa kuanza uchunguzi kuhusiana na madai ya uhalifu kutekelezwa katika idara ya uhamiaji.

Runinga ya Citizen ambayo ilifichua uhalifu huo uliobandikwa jina "Westlands undercover" ulidai kwamba maafisa katika idara ya uhamiaji na mashirika mengine ya usalama wa serikali walipanga kufukuza familia moja ya kihindi ili waweze kunyakua mali ya familia hiyo.

 Katika taarifa siku ya jumanne, msemaji Wangui Muchiri alisema Mutyambai atatoa ripoti ndani ya siku 14.

Muchiri alizidi kueleza kuwa yeyote yule pamoja na runinga ya Citizen aliye na ushahidi kuhusu suala hilo, wanaweza kufikisha ripoti hiyo kwa mkurugenzi wa kitengo cha mambo ya ndani.

Wanaweza pia kuwasilisha ushahidi huo kwa huduma ya kitaifa ya polisi, Charlton Muriithi ambaye anaweza kufikiwa kwa nambari 0798474619 au barua pepe: @nationalpolice.go.ke

Katika ufichuaji huo, kulikuwa na mpango ambao ulikuwa umepangwa vizuri kwa malengo ya kumfukuza mfanyibiashara huyo na dadake.

 Madai hayo yamemtaja naibu wa inspekta wa polisi Edward Mbugua, mkuu wa hudumu za uhamiaji Alex Muteshi, mbunge wa Makadara George Aladwa, maafisa wa DCI, na mawakili.

Ufichuaji huo ambao ulieleza na kuweka mambo wazi kuwa wahusika hao walikuwa na lengo la kuondoa familia hilo humu nchini ili wabadilishe umiliki wa mali inayomilikiwa na Dilip Bakrania na dadake Hansa Bakrania.