Je atawahi? Kipchoge ateuliwa kwa tuzo la mwanariadha bora wa mwaka

Kipchoge-hugging-his-wife
Kipchoge-hugging-his-wife
Bingwa wa dunia wa mbio za marathon Eliud Kipchoge na bingwa wa dunia wa mbio za mita 1500 Timothy Cheruiyot wameteuliwa kwa tuzo la mwanariadha bora wa mwaka wa IAAF.

Kuteuliwa kwake Kipchoge kumejia siku kadhaa tu baada ya kuandikisha historia kama binadamu wa kwanza kukimbia na kumaliza mbio za nyika chini ya masaa mawili.

Kipchoge na Cheruiyot ni miongoni mwa wanariadha 11 walio kwenye orodha iliyotolewa na IAAF kwa hafla hiyo ya kila mwaka itakayoandaliwa November tarehe 23 jijini Monaco, Ufaransa.

Wawili hao watakabiliwa na ushindano mkali kutoka kwa wamarekani Donavan Brazier, Christian Coleman na Noah Lyles.

David Rudisha ambaye ndio bingwa wa mita 800 na anayeshikilia rekodi ya mbio hizo na bingwa mara mbili wa olimpiki, ndiye mkenya pekee amewahi shinda tuzo hizo.

Rudisha alituzwa mwaka wa 2010.

Upigaji kura wa mwanariadha bora wa kiume utafungwa Novemba tarehe 4. Baadae wanaume na wanawake 5 watatangazwa na shirika la riadha duniani, IAAF.