Jumba la kifahari la staa wa zamani wa redio lapigwa Mnada

Angela
Angela
Mtangazaji  wa zamani wa redio Angela Angwenyi anakabiliwa na tishio la kukosa makao yake ya kifahari baada ya mnadishaji kuchapisha mauzo ya jumba lake katika gazeti.

Mali hiyo yenye thamani ya mamilioni ya pesa inatarajiwa kuuzwa baada ya Angela kufilisika.

Nyumba hiyo inapatikana katika bustani ya Jacaranda jijini Nairobi.

Mnamo jumatatu, madalali kutoka Garam walitangaza  kwenye gazeti  kwamba  jumba hilo ni miongoni mwa yale yanayonadwa.

Mnamo 2018, akaunti za benki ya Angela zilikuwa kati ya zilizofungwa kutokana na uchunguzi unaoendelea kuhusu kashfa ya Huduma ya Vijana kwa Kitaifa (NYS).

Akaunti ya benki ya Angwenyi ilikuwa kati ya akaunti zingine 115 ambazo zilifungwa katika benki 14 tofauti kwa kipindi cha miezi mitatu.

Mnamo 2016, alihojiwa na Kamati ya hesabu ya Bunge (PAC) kuhusu mkataba wa ushauri wa Sh milioni 302 aliyolipwa kutoka NYS.

Hii ilikuwa baada ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Edward Ouko, katika ripoti maalum ya ukaguzi juu ya akaunti ya NYS, kuhoji malipo makubwa kwa kampuni ya Angwenyi ambayo ilikuwa ni miongoni mwa kampuni zingine ambazo zilifanya biashara na huduma hiyo.