Ahmad Bahaa anafanana sana na mshambualiaji wa Liverpool na Misri Mohamed salah, na ameigiza katika matangazo mbalimbali ya televisheni.
Mhandishi Bahaa amesema katika kipindi cha runinga ya Al-Nahar TV kuwa ameshafanya matangazo ya simu na vinywaji laini akiwa ni mhusika kama Mo Salah pamoja na kampeni za kuacha madawa ya kulevya.
''Nimefanya matangazo mengi na Salah", alisema Ahmed Bahaa.
katika matangazo aliyofanya Bahaa anaonekana akiwa katika picha za mbali na sio za ukaribu sana na kuonesha sura.
''Salah kwa kweli hawezi kukaa na kufanya tangazo moja kwa muda mrefu,'' Bahaa alielezea.
''Ninachukua muda mwingi kurekodi matangazo hapa na nitaenda pia Uingereza kumalizia kurekodi naye Salah, hii ni kuharakisha mambo kwa sababu yeye hana muda mwingi wa kufanya matangazo''
Taarifa hii iliwashtua sana watu katika mitandao ya kijamii, baadhi walitumiana video inayomuonesha Bahaa katika mtandao wa Twitter.
Shabiki mmoja alishangazwa na kudhani kuwa huenda Bahaa hucheza katika michuano ya Misri akishiriki kama Mo Salah.
''Yeye ni mtu mwenye mambo mengi na Misri kila siku inafungwa huenda huyu ndo anacheza na sio Mo Salah''
Misri alikua mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Afrika lakini ilishindwa kufika Robo fainali.
-BBC