logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Je sababu ni gani?Bibi aruhusu mpango wa kando kuwa kati ya ndoa yake na mume wake

Je sababu ni gani?Bibi aruhusu mpango wa kando kuwa kati ya ndoa yake na mume wake

image
na

Habari02 October 2020 - 10:27

Ninaamini kuwa sote tunakubaliana na maneno wanawake husema kuwa hawawezi kubali mume wao awe na wasichana wengine.

Hata hivyo nilishangazwa kujua kuwa wako wanawake ambao hawana tatizo na mume wao kuwa na wanawake wengine wakidai kuwa endapo mume wake ana mawazo mengi,huyu mpango wa kando anaweza kusaidia kusuluhisha mambo kwenye boma ile.

Amini usiamini mwanamke mmoja alifunguka wazi kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa,uhusiano kati yake,mume wake na mpango wa kando uko wazi na hana tatizo lolote na maisha haya.

Aidha,mpango wa kando alisema pia,kila mara mume wa mke huyu wana tatizo,mke huyu humpigia simu na kumwomba mwanamke huyu amsaidie kusulihisha tatizo lao.

''Nimekuwa mpango wa kando kwa miaka nne sasa na wakati wapenzi hawa wako na matatizo,mimi hupigiwa simu na bibi ya huyu bwana na ninaingilia kati na kusaidia kusuluhisha tatizo hili.''

Vilevile,huyu mpango wa kando alisema kuwa,mara kwa mara huwa anaenda kuwachukua watoto wa mama huyu kama mama yao hayuko.

Aisee!Uhusiano wa wanawake hawa na mume wao ulinifurahisha kwani wao huishi pamoja kama familia na hakuna siku ambayo wao huwa na matatizo kwani bibi huyu anajua mpango wa kando wa mume wake ni nani.

Mbali an hayo,mke huyu alisema, kuwa  na wapenzi wawili si tatizo mradi tu wote wanajuana.

''Kuwa na wapenzi wawili si shida kwangu bora tu tunajuana na hakuna mwenye anasema uongo.''Bibi alisema.

Je?Wewe unaweza ishi katika uhusiano huu?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved