Naomi Ireri afunguka A-Z alivyougua ukimwi kwa tendo moja la ndoa

73246175_933080650403444_1476608034082914304_n
73246175_933080650403444_1476608034082914304_n
Mwanadada kwa jina la Naomi Ireri, 41, amefunguka jinsi tendo la ndoa mara moja lilimpa virusi vya ukimwi.

Akizungumza na kituo cha utangazaji nchini, Naomi alishiriki kimapenzi na mwanaume aliyemwacha baadaye.

"Niligundua nilikuwa na virusi vya ukimwi nikiwa na miezi mitano katika vipimo vya kliniki...

"Nilidhani nilikuwa sawa ila siku moja nikapimwa katika hospitali ya kibinafsi na kuitishwa damu yangu..."

"Walichukua (wahudumu) muda mrefu kuniita na nikaanza kujiuliza mbona wengine wanaitwa ndani na sio mimi..." alisimulia Naomi.

Naomi aliamua kwenda ndani ili aongee na muhudumu,

"Wakati nilipoingia daktari aliniuliza, ushawahi kupimwa virusi vya ukimwi? Na nikasema sijawahi...'

"Hapo ndipo niliambiwa kuwa nina virusi vya ukimwi..." Naomi.

Taarifa za kuugua maradhi ya ukimwi zilimshtua zaidi Naomi,

‘Nilijua tu ni baba mtoto alisababisha, baada ya kumpigia alisema kuwa yeye hakuwa na virusi hivyo na kunituma nikapimwe tena..."
"Sikulala siku hiyo...' Naomi
Asichokifahamu mwanadada huyu ni kuwa aliyemuambukiza ukimwi ni jamaa walifanya mapenzi kabla kupatana na mmewe.
Naomi alikutana na jamaa huyu na kujahamiana naye kabla wiki kumalizika.
Jombi huyu alimpa Kshs, 1000 na hakuwahi kumpigia tena simu.
Alipojaribu kumpigia simu hakushika simu zake.