Kundi la Ethic matatani, waomba msamaha baada ya kukashifiwa

ethic.
ethic.
Wiki iliyopita kundi la wanamziki wa Ethic walizua vurugu kati ya wananchi na bwana Ezekiel Mutua baada ya kutoa wimbo wao wa 'Tarimbo '

Wimbo huu una maneno makali sana na inasemekana kuwa, wimbo huu unatetea au kuchangia vilivyo visa vya ubakaji.

Katika huu wimbo, mwanamziki mmoja jina lake Reckless ndiye huimba,

''Mimi hupenda chapa na Tarimbo mimi huchapa na nakanyaga na namwaga bila hata permission ''

Wakenya wengi hawana tatizo na jina Tarimbo lakini wana tatizo kuu na mistari wanayosema kuwa, wanaweza shiriki ngono na binti yeyote ata bila kupewa ruhusa na binti huyo.

Mbali na wimbo huu kupata mashabiki wengi, kundi  hili la Ethic lililazimka kuomba mashabiki msamaha na bila kusita, kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wakasema,

Je baada  ya wanamziki hawa kuomba msamaha watasamehewa kweli ama bado wataenda mahakamani?