Uhuru ashambulia idara ya mahakama

UHURU KENYATTA
UHURU KENYATTA
Rais Uhuru Kenyatta amekosoa idara ya mahakama, siku moja tu baada ya Jaji Mkuu David Maraga kuishtumu serikali kwa kuidhalilisha idara ya mahakama.

Maraga siku ya Jumatu alisema kwamba atabagua hafla za serikali ambazo atahudhuria hadi pale atakapoanza kupewa heshima inayofaa wadhifa wake.

Lakini akizungumza siku ya Jumanne mjini Nairobi, Uhuru aliambia idara ya mahakama ishugulikiye kesi kwa hara ‘ikiwa inataka’

"Natoa wito kwa mahakama, wakihisi kufanya hivyo, kufanya jitihada kukamilisha kesi zinazohusisha ulipaji ushuru bila mapendeleo," alisema akicheka..

Maraga aliyekuwa amejawa na gadhabu siku ya Jumatatu aliambia mkutano wa wanahabari mbele ya majengo ya mahakama ya upeo kuwepo kwa njama ya serikali kumuondoa ofisini kabla ya mwisho wa mwaka huu.

“Baadhi ya mawari wanasema kwamba nitapigwa kalamu balaya mwisho wa mwaka huu. Kumbe hii Kenya ina wenyewe (apparently Kenya has its owners)?" Maraga alisema.