Diamond Platnumz kuiba mdundo wa ngoma ya Soapy, S2Kizzy aelezea

Producer wa mkwaju wa 'Baba Lao' ya Mondi ametokezea na kufunguka kuhusu midundo ya 'Baba Lao' na 'Soapy' ya Naira kufanana.

Akihojiwa na kituo cha Wasafi FM nchini Tanzania, S2Kizzy amesema kuwa waliomba ruksa ya kuimba na mdundo huo.

Producer huyu ameeleza kuwa alivutiwa zaidi na mdundo wa Naira katika ngoma ya Soapy.

“Wakati tukiwa Madagascar mimi Diamond. Tulienda na studio ndogo siunajua sisi ni watu wa muziki tukawa tunagonga mawe tu. Tulikuwa tumekaa tunagonga ngoma fulani slow hivi.” S2Kizzy.

“Pale tulipokuwa tumekaa palikuwa na TV inaonesha chaneli fulani hivi,  mara ikapita ngoma fulani ya Naira Marley ‘Soapy’ tukasema mbona kama ngoma ina vibe fulani hivi..Na siku tunaweza kufanya ngoma kama hii. Basi tukaona ngoja tufanye ngoma kama hii halafu tutawasiliana nao wenyewe. Kwa hiyo tukawa inspired na wimbo wa Naira Marley unaitwa ‘Soapy’, Kwa tukaona tunaweza tukaweka maneno yetu, Vibe letu na vitu vyetu lakini kwenye type ya muziki kama huo.” alisimulia S2Kizzy.

Aidha, S2Kizzy amesema kuwa ana nyimbo kama 40 zake Diamond Platnumz.

Kwenye ngoma hizi zote ni za kimataifa.

S2Kizzy anasema kuwa kuna producer wengi Afrika wanaomtafuta Diamond Platnumz.