Uchaguzi Kibra: Imran Okoth apata ushindi, Mariga ampa kongole

Imran okoth
Imran okoth
IEBC imemtangaza rasmi Imran Okoth wa ODM kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Kibra. Okoth alipata kura elfu 24,636, akifuatiwa na mwaniaji wa Jubilee McDonald Mariga aliyepata kura 11,230.

Eliud Owalo wa ANC alipata kura elfu 5,275.

Wakati huo huo Mariga amekubali kushindwa. Akimpa kongole mpinzani wake wa karibu Imran Okoth, Mariga anasema ameridhishwa na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Ushindi wa mwaniaji wa ODM Imran Okoth katika uchaguzi wa Kibra haufai kuwagawanya wakaazi wa eneo hilo. Viongozi wa ODM Ochillo Ayacko na Mohamed Sumra wanasema ingawaje kulikua na makosa ya uchaguzi, chama chao kinajitahidi kuheshimu maridhiano na uiano.

IEBC imetakiwa kujitahidi zaidi katika kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kujitokeza wakati wa chaguzi ndogo. Mkurugenzi wa shirika la HAKI Africa Hussein Khalid anasema katika chaguzi hizo chini ya nusu ya idadi ya watu hujitokeza kupiga kura. Pia anataka adhabu kali kutolewa kwa wanaojihusisha na makosa wakati wa uchaguzi.

Tumejaribu sana katika chumba cha kulala cha ODM. Haya ni matamshi ya wabunge wa Jubilee Kimani Ichungwa, Nixon Korir na John Kiarie ambao wamempongeza mwaniaji wao McDonald Mariga kwa kushindana vyema katika uchaguzi huo.