logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wafuasi wa William Ruto wapigania kutawala ngome za ODM ifikapo 2022

Wafuasi wa William Ruto wapigania kutawala ngome za ODM ifikapo 2022

image
na

Burudani02 October 2020 - 04:04
Inua Mama-compressed
Wafuasi wa naibu wa rais William Ruto wameahidi kumpigia upato na kulemaza siasa za kinara wa ODM  Raila Odinga, ambao wanasema ni "siasa duni na ya vurugu" hadi itakapotimia uchaguzi mkuu wa 2002.

Kikundi cha Inua Mama, gavana wa  Uasin Gishu  Jackson Mandago pamoja na wabunge  Oscar Sudi na Caleb Kositany wamesema kwamba wanaimarisha kampeni zao katika ngome za Jubilee.

Vikundi hivi vilifanya mikutano katika maeneo ya Eldoret na Iten Jumamosi huku wakiangazia juhudi zao dhidi ya kinara wa ODM.

Wabunge Sudi na Kositany walimshtumu Raila na  chama cha ODM kwa ghasia zilizoshuhudiwa Kibra Novemba 7, katika uchaguzi mdogo wa eneobunge hilo.

"Tumekubali kwamba mgombeaji wa chama chetu alishindwa katika uchaguzi wa Kibra ila tunamwahidi Raila Odinga hatashinda uchaguzi mkuu wa 2022. Tulivamia Bedroom yake kuchukua kila kitu isipokuwa godoro, ila tutaiendea hivi karibuni," Sudi alisema.

Kositany na Mandago walisema kwamba vurugu katika Kibra hulemaza juhudi za demokrasia zilizoafikiwa nchini.

Aidha walisema hawatawapata fursa timu ya Raila kutumia nguvu kuingia madarakani.

Sudi alisema kwamba fujo na ghasia katika Kibra in ishara kwamba BBI iliundwa ili kuwahadaa Wakenya bali siyo kuleta maridhiano na uwiano.

Miongoni mwao ni wabunge wanawake Jane Kihara wa Naivasha, Cate Waruguru  mwakilihi wa wanawake Laikipia, Jane Nangabo wa Trans Nzoia, Purity Ngirici  mwakilishi wa wanawake wa Kirinyaga na  Gladys Shollei ambaye ni mwakilishi wa wamama wa Uasin Gishu.

Wanawake hao walimsihi waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kustaafu katika siasa huku wakimshtumu kuwa kizingiti kikuu cha siasa za Kenya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved