Babu amesema kuwa kuna watu asiowajua wanaotaka kumtoa uhai.
Kulingana na mwanasiasa huyu shupavu, gari aina ya Saloon inamfuata aendapo na hivi anahofia sana kuwa kuna njama ya kumuangamiza.
"Najulikana kwa kuwatetea watu wa kawaida bila woga.Jambo hili linaonekana kuwakera watu wenye mamlaka makubwa visivyo...," kipande cha kauli kiliandikwa.
"Na nikimaliza,sitakoma. Lazima mauti yamkute kila mtu na siku yangu itafika.Siogopi kufa kwa kile ninachokiamini na kuwatumikia watu wangu. Tialala!"
Owino amevitaka asasi za usalama na Inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai kuzidisha juhudi katika za kuchunguzi kisa hicho.