Matokeo ya mtihani wa KCPE kutangazwa muda wowote, wizara ya elimu

knec
knec
Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) yanatarajiwa kutangazwa leo, afisa mmoja wa wizara ya elimu amesema.

Afisa huyo amesema washika dau wa elimu wanakutana kwa sasa katika makao makuu ya baraza la mitihani nchini KNEC jijini Nairobi kujadili matokeo hayo.

Kwa sasa washikadau wa wizara ya elimu washaanza kuwasili katika katika makao makuu ya KNEC.

Waziri wa elimu Prof George Magoha anatakiwa kumtaarifu Rais Kenyatta kabla ya matokeo haya kutangazwa.

Jumla ya wanafunzi 1,088,986 walifanya mtihani wa KCPE mwezi jana.

Usahihishaji wa karatasi za Insha na kizungu ulimalizika Ijumaa.

Zaidi ya watahiniwa milioni moja wanatarajiwa kupokea matokeo yao siku 18 pekee tangu kumalizika kwa mtihani huo.

Waziri wa elimu George Magoha alikuwa tayari ameahidi wazazi kuwa matokeo ya mtihani huo yangetolewa mapema kabla ya siku ya Krismasi.

Kama ilivyo katika kanuni mpya orodha ya matokeo ya shule haitatolewa bali ni wanafunzi waliofanya vyema pekee watakaotajwa.

Punde tu baada ya kutolewa kwa matokeo haya, wizara ya elimu itaanza mchakato wa kuchagua shule.