(+ Video ) Uhuru Kenyatta aangua kicheko kisa kauli ya Junet, Ruto hakupendezwa

1_51__1574925892_89027
1_51__1574925892_89027
Kipande cha video kinachomwonyesha Rais Uhuru Kenyatta akicheka tamko la mbunge Junet kimewafurahisha wengi katika mitandao ya kijamii.

Junet alikuwa mfawidhi (Mcee) katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya BBI hapo jana Jumatatu.

Kabla kumkaribisha kiongozi wa wengi bungeni, Junet alionya kuwa mtu yeyote asilete matatizo ya chama cha Jubilee katika hafla ya kitaifa.

Rais Uhuru Kenyatta aliangua kicheko kikubwa.

https://www.instagram.com/p/B5XlH9epUZ_/

Makamu wa Rais William Ruto alionekana kutopendezwa na kauli hiyo.

Baadaye Murkomen alifika jukwaani na kuanza kuhutubu.

Murkomen alinyamazishwa na hadhira baada ya kutilia shaka jinsi maoni kinzani katika ukumbi huo yalilengwa.

“Mimi kama kiongozi lazima niseme, siwezi kusimama hapa nitarajiwe kupigia upato siasa mbaya. Waandalizi wa hafla hii wameipanga kwa njia ambapo watu wenye maoni tofauti wamefungiwa nje,” alisema Murkomen.