Shamte mume wa mama Diamond asimulia walipokutana, akana taarifa za kumuoa kisa hela

diamond-mum
diamond-mum
Shamte ambaye ni mume wa mama Diamond amefungua sehemu na ambapo alikutana na mama huyu.

Akipiga story na Bongo 5, Shamte aidha amepuuzilia mbali ubuyu kuwa alikwamilia kwa mama Diamond kisa hela,

"Kwa jinsi unamwona huyu bibiye wewe, ushawahi kumskia akaonga mtu?Hakuna mtu anapata hela kwake yeye. Bibi huyu alikuwa rafiki yangu,urafiki ukatengeneza mahusiano, mahusiano yakatengeneza mke na mume...' Alianza kusimulia.

Shamte amesema kuwa yeye na Sanura walikutana mjini Paris,

"Na tulikutana Paris, muulize yeye ndo anajua ila mtu akataka kuzungumza azungumze..."

Mume huyu amesema kuwa kumpata mama Diamond zilikuwa baraka tele,

"Kwanza nilikuwa sijawahi oa katika maisha yangu na yeye alikuwa hajawahi kuolewa katika maisha yake kwa hivyo tumejipata wote wapya kwenye ndoa kwa hiyo nashukuru mungu..."

Shamte amesema kuwa hachukii wakati na ambapo media zinawaandika kuhusu uhusiano wao

"Kwanza tunacheka, kwani wakati huwa tunapenda, tunajua na watu watuongelea vipi tusije tukajiona tuko sawa kumbe hatuko sawa..."