Tendo moja la ndoa lamsababishia virusi vya UKIMWI, Ireri afunguka A-Z

92afb4dc_819d_4964_aaec_48e3a2b89f2f__1573481672_68154
92afb4dc_819d_4964_aaec_48e3a2b89f2f__1573481672_68154
Mwanadada kwa jina la Naomi Ireri, 41, amefungukia Massawe Japanni jinsi tendo la ndoa mara moja lilimpa virusi vya ukimwi.

Akizungumza na kipindi kinachoruka kituo hiki cha Bustani la Massawe, Naomi alishiriki kimapenzi na mwanaume waliojuana kwa kipindi cha wiki mbili.

Baada ya mwaka mmoja, Naomi alipata mwanamume mwingine na akazaa naye mtoto bila kujua alikuwa tayari ashapata virusi vya UKIMWI.

“Niligundua nilikuwa na virusi vya ukimwi nikiwa na miezi mitano katika vipimo vya kliniki…

“Nilidhani nilikuwa sawa ila siku moja nikapimwa katika hospitali ya kibinafsi na kuitishwa damu yangu…”

Taarifa za kuugua maradhi ya ukimwi zilimshtua zaidi Naomi,

‘Nilijua tu ni baba mtoto alisababisha, baada ya kumpigia alisema kuwa yeye hakuwa na virusi hivyo na kunituma nikapimwe tena…”
“Sikulala siku hiyo…’ Naomi.

 Asichokifahamu mwanadada huyu ni kuwa aliyemuambukiza ukimwi ni jamaa walifanya mapenzi kabla kupatana na mmewe.
Naomi alikutana na jamaa huyu na kujahamiana naye kabla wiki kumalizika.
Jombi huyu alimpa Kshs, 1000 na hakuwahi kumpigia tena simu.
Alipojaribu kumpigia simu hakushika simu zake.

"Tulifanya sex baada ya kumwambia asimwage ndani."

Baada ya kufanya mapenzi na jamaa huyu, mawasiliano yalikata ghafla.

"Akanyamza nikaona amenimwagia. Ningejua ni ukimwi ningeenda hospitali nipewe dawa ya kuzuia HIV..." Alisimulia Ireri.

"Nikampigia simu hashiki ,jumbe akawa hajibu na nikaamua kunyamaza nikasahau hiyo story..."

Kinachomshangaza Ireri ni kuwa mwanamme waliyezaa naye mtoto hakupatwa na UKIMWI.

Ireri alichukulia hali yake kijasiri na akaamua kusomea elimu ya kilimo.

Kwa sasa, mwanadada huyu ni sauti ya watu wanaoishi na UKIMWI.

"Nilikaa nikaona vile niko bold nijitokeze nikaelewa na nika-jiencourage. Watu watumie condoms..."

Naomi amesema kuwa unaweza ukampigia simu kwa namba 0722384881 au utume arafa mtotowaafrica23@gmail.com ili aweze kukuhimiza kuhusu kuishi na virusi vya UKIMWI.