Miji mikuu 10 bora zaidi barani Afrika

Accra-Ghana
Accra-Ghana

Ijapokuwa bara la Afrika limedhamiriwa kuwa na umaskini zaidi ulimwenguni na kutazamwa kama bara lililo gizani, kunayo baadhi ya miji mikuu ambayo hukufanya kufikiria zaidi kuhusu taswira hiyo.

Hii ni miji mikuu 10 inayoaminika kuwa bora zaidi Afrika kutokana na upekee wao unaojitokeza.

Nairobi

Nairobi ni Mji Mkuu wa Kenya na kubwa zaidi katika Afrika Mashariki. Pia ni miongoni mwa miji inayokuwa haraka kisiasa na kifedha katika bara la Afrika. Nairobi ni nambari 4 Afrika katika sekta ya kibiashara.

Cape Town

Ni mji mkuu wa taifa la Afrika Kusini. Jiji hili ni maarufu sana kutokana na mandahri yake mazuri yanayopakana na upwa wa Bahari, pia inajulikana kutokana na utamaduni wake wa upekee.

Accra

Ni mjii mkuu wa Ghana. Ni maarufu kutokana na raha za nyakati za usiku, masoko ya kitamaduni, makavazi, na upwa za bahari zinazong'aa.

Johannesburg

linajulikana sana kama Jorburg. Ni kubwa zaidi katika Afrika Kusini na la pili katika Africa nzima. Jiji hili lina utajiri mkubwa sana Afrika Kusini kwa ukuaji wake wa kiuchumi, kimawasiliano, kisiasa, usafiri na uchimbaji wa madini.

Lagos

Ni mji mkuu wa Nigeria.

Umaarufu wake hutokana na hidaya nzuri na mavazi ya Agbada, sherehe za burudani usiku pamoja na filamu na sinema. Inapatikana katika ufuo wa bahari ya Atlantiki na ni miongoni mwa miji inayovuma kutokana na sanaa za utamaduni na kazi za ufundi.

 

Dar es Salaam

 

Awali lilikiwa jiji kuu, jiji la Dar es Salaam linapatikana katika pwani ya uswahilini.

Ni maarufu kutokana na mapishi ya kipwani, mlima Kilimanjaro na mbuga za wanyama.

Cairo

Ni mji mkuu wa Misri.

Ni mojawapo ya miji ya kale zaidi Afrika na inafahamika kutokana na piramidi za kale na uhifadhi wa sanaa za kifalme.

Pia ni maarufu kwa mandhaari mazuri.

Kigali

Ikiwa imezungukwa na milima na mabonde, Kigali ni mji mkuu wa Rwanda.

Ni jiji safi sana barani Afrika. Inajulikana kwa mikahawa na sherehe za burudani usiku.

Mbali na hayo, ina makavazi ya makumbusho ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Addis Ababa

Ni mji mkuu wa Ethiopia. Ni maarufu kwa sanaa ya kitamaduni, makavazi na mabaki ya viungo vya kabla ya kihistoria.

 Casablanca

Ni mjii mkuu wa Morocco.

Ni muhimu sana katika Afrika kiuchumi, kidemografia na kimandhari.

Casablanca ni mji maarufu kutokana na mikahawa ya kienyeji kama vile Sheesha , makavazi, ufuo za bahari Mediterranean na sherehe za usiku.