Kenya hadi Bongo: Collabo 5 bora zaidi mwaka huu

collabo
collabo
Mwaka wa 2019 umekuwa wa kufana sana katika sekta ya sanaa nchini kwani kando na miaka iliyopita, wasanii wetu wamejikakamua kisabuni. Kutoka wasanii waliokithiri, kina Khaligraph, Sauti Sol, Nameless, Wahu hadi wasanii wa kizazi kipya kina; Ethic, Ochungulo family na Sailors wote wameonesha ubabe wao kupitia nyimbo walizozindua.
Isitoshe, baadhi yao wameonesha uhodari wao na kuvuka mipaka ambapo wameweza kufanya collabo na wasanii kutoka mataifa jirani, huku Tanzania ikiwa kivutia kikuu cha wasanii hawa.
Radio Jambo hii leo tunakupa orodha ya collabo kumi bora zilizofanywa na wasanii kutoka Kenya na Bongo mwaka huu.
1. Nandy ft Sauti Sol - Kiza Kinene
Kusema wimbo huu ulizinduliwa wiki moja tu iliyopita na kulingana nami, tayari huu ni wimbo wa mwezi! Nandy amewashirikisha magwiji hawa wa Afrika na kuonesha upande tofauti sana, kwani watu wamezoa nyimbo zao huwa za party ama zimejaa vidosho wenye makalio kweli.
Wimbo huu tayari umetazamwa zaidi ya mara milioni moja, Youtube.

2. Nandy willy paul - Hallelujah
Kwa mda sasa, kumekuwa na tetesi kuwa Willy Paul ambaye sasa hivi ni bayana kuwa sio msanii wa nyimbo za injili, anachumbiana na Nandy. Hili lilifuatwa na collabo murwa kwa jina Hallelujah ambayo hadi sasa hivi imeshika Kenya na Tanzania na kama kawaida, Nandy aliwakilisha Bongo vilivyo.
Video ya wimbo huu tayari imetazamwa zaidi ya mara milioni saba.

3. Ali kiba Ommy Dimpoz, Willy Paul - Nishikilie
Willy Paul ambaye tayari amekuwa na mwaka wenye mafanikio mengi kimziki licha ya scandal kibao, alishirikiana na King Kiba na mwenzake kutoka Tanzania bwana Ommy Dimpoz kwenye kibao hiki.
Watatu hawa ambao ni marafiki sugu wa gavana wa Mombasa, mheshimiwa Hassan Joho, waliwapa wanadada kibao cha kunengulia viuno na ambacho kimewateka wengi.
Hata hivyo, video ya ngoma hii haikuvuma sana kwani imetazamwa mara milioni moja nukta tano pekee kufikia sasa.
4. Rose Muhando Ringtone - Walionicheka

Wimbo huu ambao unatumika kama ushuhuda wake bi Muhando baada ya kupambana na ugonjwa kwa siku nyingi, unamshirikisha bwana Ringtone kutoka humu nchini. Ringtone amabaye amekuwa akigonga vyombo vya habari kwa mda, kwa sababu ya mambo ayafanyayo kwenye mitandao ya kijamii, anasifiwa sana na mashabiki kwa ustadi wake.

Wimbo huu ambao ulizinduliwa wiki moja pekee iliyopita, umetazamwa mara 750,000.

5. Willy Paul Ft Rayvanny - Mmmh
Miezi sita sasa tangu wawili hawa wazindue wimbo huu, wakenya na watanzania bado wanaupenda kwa ustadi na upole wake. Wimbo huu ambao unazungumzia tu mapenzi yao kwa wapenzi wao tayari umetazamwa zaidi ya mara milioni kumi.

6. Gabu Ft Mbosso - Mastory
Gabu ambaye kitambo alikuwa wa kikundi cha P-Unit alirudi na kishindo mwaka huu, yeye pia akimshirikisha mtanzania kwa jina Mbosso mwezi Januari. Wimbo huu licha ya kuchezwa sana kwenye klabu humu nchini, ulitizamwa mara milioni moja pekee.

Baadhi ya nyimbo zingine ambazo ziliwashirikisha wasanii kutoka mataifa haya mawili, ni Wakati wa mungu wimbo wake Paul Clement na Guardian Angel na Bahati ft Mbosso - Futa, nyimbo ambazo pia zilionesha ushirikiano mwema dhidi ya wasanii kutoka mataifa haya.