Afisa wa polisi anyofolewa sehemu za siri na mke wake

IMG_0846 (1)
IMG_0846 (1)
Maafisa wa polisi wanadadisi kwa jicho pevu kisa na ambacho mwanadada Frola Adamu anatuhumiwa kukata sehemu za siri za mume wake.

Kisa hiki kinatajwa kufanyika mtaa wa Shinyanga nchi jirani ya Tanzania.

Kauli ya polisi inasema kuwa tukio hilo la kinyama lilitokea Disemba 28 mwaka jana.

Dada huyu anashukiwa kumkata mumewe nyakati za usiku.

Jamaa huyu ambaye ni afisa wa polisi alikuwa amelala na mke wake kikawaida wakati na ambapo kisa hiki kilitendeka.

Akimvamia kwa kisu kikali, mwanadada huyu anadaiwa kumjeruhi vibaya na kumnyofua sehemu zake nyeti.

“Baada ya askari huyu kukatwa uume wake alikimbizwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ili kupatiwa matibabu ya haraka, ambapo alilazwa kwa muda wa siku mbili na kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea kujiuguza na kidonda,”alisema afisa wa polisi nchini humo.

Migogoro ya kimapenzi inakisiwa kuwa sababu kuu ya tukio hili.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi, ambapo mwanamke alikuwa akimtuhumu mumewe kuwa ana nyumba ndogo, ndipo akaamua kuchukua kitu chenye ncha kali na kisha kuanza kuukata uume wa askari na kumjeruhi vibaya,”aliongeza afisa huyo.