logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkimbia uchi usiku asimulia siri za familia anazotembelea,ajisifia kwa mbio

Mkimbia uchi usiku asimulia siri za familia anazotembelea,ajisifia kwa mbio

image
na

Habari02 October 2020 - 04:36
Vz2xe4zsARNight-runner-in-the-act-696x365
Mkimbiaji wa usiku amepiga simu kukiri kuwa ana siri za boma nyingi katika kijiji chake.

Jamaa huyu alipiga simu katika kipindi cha Mbusi Na Lion TekeTeke na kusema kuwa anaweza kutaja wanandoa wasiofanya tendo la ndoa.

"Eeh naweza kujua watu ambao hawajatamba ama wametamba (Kushiriki ngono)..."

Jamaa huyu aliwashangaza Mbusii Na Lion kwa kusema kuwa anafahamu siri nyingi za familia.

Watu wanaokimbia usiku wametajwa sana kuwa na chimbuko la Magharibi mwa Kenya.

Jamaa hawa wana uwezo wa kukimbia kwa giza bila kuonekana.

Iwapo watapatikana wanaweza toa chochote ili kujinusuru.

Watu hawa wana sifa za kusumbua watu wanapolala nyakati za usiku.

Akifungukia kitengo cha Toboa Siri, jombi huyu alisema kuwa mbio zake ni sawa na za mkimbiaji na nyota wa ridha Usain Bolt.

"Ata Usain Bolt hawezi kuniacha....' Aliisimulia Toboa Siri

Kipindi hiki huwa kinaruka kila siku (Jumatatu- Ijumaa) hadi saa moja kamili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved