(+Video )Benjamin Washiali ajitetea kuhusu video aliyopiga mtu

HfvTzy5LI8DghxCIvXUAETK2d
HfvTzy5LI8DghxCIvXUAETK2d
Mbunge wa Mumias mashariki Benjamin Washiali amekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa kuwa alimpiga na kumjeruhi kijana barobaro kwenye video inayosambaa kama moto jangwani.

Kipande hicho kifupi cha video hiyo kinamwonyesha Mbunge Benjamin Washiali akimchapa mwanamume mwingine.

https://twitter.com/amerix/status/1213850734502010881

Washiali anaonekana akimshambulia kwa ngumi na mateke.

Benjamin amejitetea kuwa tukio hilo lilifanyika mwaka wa 2015 na jamaa anayemchapa alifumaniwa akiiba mafuta.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walijawa na hamaki huku wakimtaka Washiali kujiuzulu.

"Hii ni video ya zamani mwaka 2015, sio ya sasa. Nilijawa na ghadhabu baada ya kumpata mwanamume mmoja akivuja mafuta kutoka kwa moja ya trekta inayohudumu katika shamba moja la miwa," alijitetea mbunge huyu.