Hatimaye Tanasha Donna afunguka kuhusu kuchepuka kwa Diamond Platnumz

rqnkunybkva8523nsb5c00dd272cf46
rqnkunybkva8523nsb5c00dd272cf46
Staa wa kike hapa nchini Tanasha Donna hatimaye amefunguka kuhusu uvumi unaosambaa kumhusu Diamond.

Vyanzo mbalimbali vya udaku vilikuwa vinahoji kuwa huenda mwanamuziki huyo akawa anachepuka au ana jicho a nje.

Simba anatuhumiwa kutoka kimapenzi na mwanadada kutoka Tanzania.

Tanasha amewataka watu kukoma kusambaza uvumi na ambao hawajashuhudia kwa macho yao.

Kuzungumziwa kwa swala hili kumemfanya Tanasha kuwajibu wafuasi.

https://www.instagram.com/p/B6_IjvCAp3R/

Story za Chibu Dangote kuchepuka zinajiri muda mchache baada ya kusema kuwa atamuoa Tanasha.

Kwa kile kinachoonekana kuwa somo kutoka kwa wanandoa na sherehe nyingi zinazofanyika nchini humo, Simba ameamua kufanya harusi na Tanasha Donna.

"Naomba mwenyezi Mungu atubariki. Mungu akipenda mwaka ujao itakuwa zamu yangu. Karibu kila mtu ninayemfahamu hapa ameoa kwa hivyo sina sababu ya kusema sitaoa pia. Nina mwanamke mzuri ambaye amenipa mtoto mrembo na sikosi chochote kutoka kwake..." Alisema Diamond Platnumz.

Mondi alisema tamko hili katika sherehe za ndoa ya dadake Queen Darleen.

Haya yalijiri baada ya staa huyu kuchapisha video katika mtandao wa Insta akionyesha mapenzi ya dhati akiwa na mrembo Tanasha.

Tanasha amesema kuwa uhusiano wake na Diamond huwezi kukatishwa na uvumi mbaya.