PICHA YA SIKU: Manang'oi amzawadi Ghost Mulee na viatu vya riadha

manang.oi.1
manang.oi.1
Bwana Ghost Mulee ni gwiji wa kadanda humu nchini na katika fani yake yeye amefanya urafiki na ma gwiji wengi kutoka nyanja mbalibali, humu nchini na hadi ng'ambo.

Miongoni mwa marafiki hao nikutoka nyanja ya riadha na marafiki wake wa dhati ni Asbel Kiprop na Elijah Manang'oi ambaye ndiye anashikilia ubingwa wa mbio za mita 1500 za Commonwealth na pia ubingwa wa Africa nzima.

Hapo jana akiwa katika harakati zake za kadanda, bwana Ghost Mulee alipatana na Manang'oi na gwiji huyo akamtunuku viatu murwa kabisa vya riadha kutoka kampuni ya Nike.

Kupitia mtandao wake, Ghost alimshukuru Manang'oi akimuombea baraka tele.

Alisema,

Thank you 1500 mtrs World, Commonwealth,African champion for this Nike running shoes. God bless a giving heart.Thanks Inspector Elijah Manangoi for the shoes.

https://www.instagram.com/p/B7UHjD4F8yc/