Moi hakuwai kuzungumza kuhusu umuhimu wa rungu hiyo lakini chimbuko la kuwa nayo ni kutoka jamii yake ya Tugen huko Baringo ambapo vijana hushauriwa na wazee kutemebea na angalau silaha ya kujilinda dhidi ya wanyama wa msitu ." Kuanzia akiwa mdogo ,Moi alikuwa akijihami kwa rungu ,mshale au kisu ili kujilinda dhidi ya wanyama hatari kama vile Chui , sokwe au mwewe ‘ Ameandika Andrew Morton aliyeandika wasifu wa Mzee Moi kwa jina -Moi, the Making of an African Statesman'', kitabu ambacho kilichapishwa mwaka wa 1998 .