(+Picha na video)Tuju afanyiwa upasuaji baada ya kuhusika katika ajali .

Katibu wa chama cha Jubilee  Raphael Tuju  amefanyiwa upasuaji katika hospitali ya  Kijabe akabla ya kusafirishwa hadi katika Hospitali ya Karen kwa matibabu baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani eneo la  Magina  kwenye barabara kuu ya Nairobi kwenda Nakuru .

Afisa mkuu mtendaji wa Hospitali ya Kijabe  Ken Muma  amesema hawawezi kufichua lolote kwa sababu ya familia na jukumu la hospitali kulinda usiri wa wagonjwa .Tuju  alikimbizw akatika hospitali ya  AIC Kijabe  pamoja na mlinzi wake na dereva na wasamaria wema baada ya  ajali hiyo iliyohusisha matatu walipokuwa wakienda Kabarnet ,Nakuru kwa maazishi  ya Marehemu Mzee Daniel Moi .

Tazama video ya Tuju akiingizw akatika hospitali ya Karen .

https://twitter.com/YusufJumaKenya/status/1227594300768358400

Gari la Tuju  liligongana na matatu yachama cha ushirika cha  Nuclear Sacco,  iliyokuwa ikija Nairobi .  Gavana wa Machakos Alfred Mutua ,waziri wa Spoti Amina Mohamed,waziri wa ICT Joe Mucheru  na waziri wa Uchukuzi James Macharia walimtembelea  Tuju hospitalini .