Tanzia: MCA wa Kiambu Cyro aaga dunia India

cyrus omondi
cyrus omondi
 Mwakilishi mmoja wa bunge la kaunti ya Kiambu ameaga dunia akiwa katika ziara ya kikazi nchini India . mwakilishi huyo wa wadi ya kahawa Wendani  Cyrus Omondi ameriotiwakuaga dunia baada ya kukumbwa na mshutuko wa Moyo ,amesema spika wa bunge la kaunti hio Stephene Ndichu .

Ndichu  amesema mwakilishi huyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya unge la kauti kuhusu elimu alikuwa na wenzake wakati wa warsha kuhusu  ya elimu alipofariki katika chumba chake .

Omondi,  alikuwa kiongozi mchangamfu  ambaye alishindatiketi ya jubilee ili kuliwakilisha eneo hilo  licha ya kuwa ni  mwenyeji wa Kauti ya Siaya na kufaulu kushinda kiti katika  kaunti yenye idadi kubwa ya watu wa jamii ya kikuyu .

Kifo chake kimewatamausha wengi kwani inaripotiwa  kwamba alikuwa katika hali nzuri ya  kiafya . Wenyeji walikuwa walimwita kwa majina ya utani ‘Cyro’ au ‘Gearbox’.