Dennis Okari na mkewe Naomi washerehekea mwaka mmoja tangu wafunge ndoa 

Mwanahabari Dennis Okari na mkewe Naomi, tayari washerehekea mwaka mmoja tangu wafunge pingu za maisha. Kama kweli muda hukimbia!

Huku wengi wakiendelea kusherehekea wikendi ya wapendanao, Okari aliandika ujumbe kwa mtandao wake wa insta akisema:

I’ve waited this long to say happy 1st anniversary to you, my love. I cherish, respect, and honor you on this special day. You are the most amazing woman of God I’ve come to know. To many more years together. To many more celebrations.

To God, thank you for giving me the Joy of my life. To our church @chrisco_upper_room_fellowship thank you for praying with us. To our family and friends, thank you for supporting us and walking with us.

To the amazing @luxeallureevents you gave us the best wedding gift in the decor and we were delighted. Thank you all for the birthday wishes as well. #weddinganniversary #marriageworks

Sherehe hizi zajiri miaka kadhaa baada ya ndoa yake Okari na mwanahabari mwenza, Betty Kyallo kutibuka.

Wawili hao walijaliwa mtoto mmoja wa kike.

Hata hivyo, kila mmoja aliondoka na kwenda zake huku wakifanikiwa kupata wapenzi wapya huku wakiendelea kumlea mwana wao pamoja.

Sisi kama Radiojambo.co.ke tunawapongeza wapenzi hawa na kuwatakia maisha bora yaliyojaa upendo.