Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema kwamba Mburu alifariki siku ya Jumapili kutokana na maradhi ya mshtuko wa moyo.
Kulingana na wizara hiyo, balozi aliondoka nchini siku ya Jumapili akielekea mjini Juba kabla ya tukio hilo.
"Kile twajua kwa sasa ni kwamba balozi alipatwa na mshtuko wa moyo. Tunajaribu kupata maelezo zaidi na tutatoa taarifa kamili baadaye.taarifa kutoka kwa wizara hiyo.
afisa mmoja wa wizara ya mashauri ya nchi za nje alisema.
Wizara ilisema Mburu alikuwa nchini alipoandama na rais Salver Kiir kuhudhuria mazishi ya hayati rais mustaafu Daniel Moi.
Duru nchini Juba zilisema kwamba Mburu aliwasili kutoka mjini Nairobi siku ya Jumapili na kwenda hospitalini moja kwa sababu alikuwa hahisi salama.
Hali yake haikuwa mbaya zaidi na kwamba hali yake ilikuwa thabiti.
‘’Uchunguzi wa mwili wake waonyesha kuwa “kiwango cha shinikizo la damu kilikuwa juu, hatua inayoashiria tatizo katika ini lake” duru ziliarifu.