Picha ya siku: Jamaa afunga harusi akiwa amevalia sare ya Arsenal

Jamaa mmoja amewashangaza wengi na kufurahisha wengine baada ya kuchapisha picha zake na mkewe mtandaoni, baada ya kufunga harusi.

Kilicho shangaza na kufurahisha ni kuwa kinyume na bwana harusi wengi ambao huvalia suti, yeye aliamua kuadhimisha siku hiyo akiwa amevalia sare za Arsenal.

Ni dhahiri kuwa jamaa huyo ni shabiki sugu wa Arsenal na licha ya timu hiyo kuwa na msimu mbaya, aliamua hilo halitamzuia kufurahia harusi yake na timu anayoipenda.

Isitoshe alihakikisha kuwa amevalia sare ya Arsenal ya nyumbani (nyekundu) na ya ugenini (njano)

Alichapisha picha zile na ujumbe uliosema; I Love you home & away (Nitakupenda nyumbani na mbali na nyumbani au ugenini). Kisoka, timu zote duniani lazima zicheze mechi dhidi ya mahasimu wao, nyumbani kwao na pia ugenini.

Tazama picha zifuatazo;