Ni kubaya! VP wa Iran aambukizwa virusi vya Corona .

IRAN VP
IRAN VP
  Makamu wa rais wa taifa la Iran Masoumeh Ebtekar,  ambaye pia anasimamia masuala ya wanawake na familia  amepatikana na virusi vya  Corona . Makamu huyo ambaye pia anajulikana kama  msemaji wa kiingereza wa watekaji nyara wa mwaka wa 1979 katika ubalozi wa Amerika nchini humo  na kusababisha mgogoro wa kidiplomasia uliodumu siku 444  alipimwa na kupatikana na daalili za virusi hivyo .

Siku ya jumanne maafisa wa Iran walithibitisha kwamba  naibu waziri wa afya Iraj Harirchi  alikuwa pia ameambukizwa virusi vya corona na aliwekwa katika wadi ya kutengwa  kwa uangalizi .

Taifa hilo limefutilia mbali mahubiri ya siku ya ijumaa  katika mji mkuu Tehran  na kote nchini . hatua hiyo imechukuliwa baada ya ongezeko la haraka na la kuhofisha la watu walioambukizwa kutoka idadi ya watu 100 hadi watu 246 huku vifo 26 vikithibitishwa . Iran Pia imewapiga marufuku raia wa China kuingia nchini humo .