Diamond atokelezea na mavazi ya ajabu baada ya kumtema Tanasha

Zaidi ya siku tatu zilizopita Diamond amekuwa akienea sana katika mitandao ya kijamii kwa ajili ya uhusiano wake na Tanasha hii ni baada ya Tanasha kusema kuwa Diamond hana heshima wala haaminiki.

Tanasha alitoka nchini Tanzania na kurudi nchini Kenya baada ya kuzuiwa kwenda na Diamond ng'ambo.

Ni jambo ambalo liliibua hisia mbali mbali miongoni mwa mashabiki, kuhusu uhusiano wa wawili hao, hata mwezi hujaisha baada ya kutoa wimbo wao wa 'Gere'

Diamond ni mwanamuziki ambaye watu hutarajia chochote kutoka kwake endapo yupo jukwaani akiimba ama yupo hadharani akihutubia mashabiki wake.

Wawili hao walitengana huku meneja wa lebo ya WCB akisema sababu kuu ya hao wawili kutengana ni kukoseana heshima.

Jana Diamond alikuwa na mkutano katika hoteli ya Serena na mashabiki wake walikuwa tayari kujua ni nini kilijiri katika uhusiano wake na Tanasha na uamuzi wake ni upi.

Diamond  alifika jukwaani kama hajavalia shati lakini alikuwa amevalia koti lenye la maua ya kijani kibichi.

Mmmh ni jambo ambalo si la kawaida sindio? msanii kama yeye alikuwa anatarajiwa kupanda jukwaani akiwa amepiga pamba ya hadhi yake kuwahutubia watu.

Baada ya muda mfupi Simba alienda kuvaa shati na kutokelezea jukwaani kama amevalia nadhifu ishara kwamba meneja wake hawakupendezwa na mavazi hayo.

Na pia kumkumbusha kuwa anatoa hotuba yake kwa watu wengi na maalumu mbali si muziki anatoa ama anaimba.

Diamond alipoulizwa kuhusu kipenzi chake Tanasha hakujibu swali lolote, kweli simba ni yule yule.

Cha maana ambacho Diamond alisema jukwaani ni kuwa amekuwa balozi wa corol paint nchini Tanzania.

Je wawili hao watatatua mambo au Tanasha aanze msafara wake kama wale wanawake wengine waliokuwa katika maisha ya Simba?