"Don't ever play with our Tanasha," Gidi amuonya Diamond

diamond (1)
diamond (1)
Hii leo kabla ya kitengo cha Patanisho, Gidi alizungumzia kuhusu uhusiano uliotamatika baina ya mwanamuziki Diamond Platnumz na mkenya Tanasha Donna.

Gidi alisema kuwa amekuwa akishawishiwa na mashabiki wa Radio Jambo ajaribu kuwapatanisha wawili hao kabla ya maji kuzidi unga.

Kwa upande wake, mtangazaji huyo aliwajibu,

"Ngoja ngoja, tunaipanga panga tunaipika na tukipata Diamond yuko available na Tanasha Donna yuko available hapa nchini ama kule Tanzania, tutapiga simu na tuone kama tutaweza kuwapatanisha. " Alisema.

Aliongeza,

Hata ingawa zile habari napata ni kwamba huyu Tanasha ndiye alimuacha Diamond. Tafadhali Diamond baada ya press conference nitumie Whatsapp vile wewe hunitumia na mara moja nipange vile nakupatanisha na huyu msichana wetu."

Isitoshe, Gidi hakusita kumkanya Diamond kutocheza na moyo na akili zake Tanasha haswa ikizingatiwa ni mrembo kutoka humu nchini.

Na tafadhali, don't ever play with our girl!