Sauti Sol, Nameless na Kidum wananitafuta tufanye collabo - Ghost Mulee

67572951_122315605801944_5858248206995081202_n
67572951_122315605801944_5858248206995081202_n
Staa na nyota wa utangazaji nchini Ghost Mulee sasa anahoji kuwa baadhi ya mastaa nchini wanamtafuta ili wapate kumshirikisha katika nyimbo zao. Tamko hili alilifanya kiutani sana huku akisema sauti yake ni kali sana ana uwezo wa kuimba.

https://www.instagram.com/p/B2D_vMoldef/

Ghost alichukua nafasi hii adimu sana kumwimbia mwenzake Gidi na kumtakia heri njema katika sikukuu ya kuzaliwa kwake mapema wiki hii.

Soma hadithi nyingine:

Gidi alizaliwa miongo kadhaa iliyopita na kila mwaka yeye huhakikisha kuwa amejivinjari vilivyo lakini kitu ambacho hupenda kufanya ni kusafiri hadi Ufaransa kuitembelea familia yake kwa siku kadhaa.

Mwaka uliopita, Gidi alifanya jambo la busara sana kwani alipanga sherehe ambayo aliwaalika marafiki zake na wakuu kutoka nyanja mbali mbali humu nchini.

Sherehe hiyo iliyo andaliwa katika hoteli ya Ole Sereni, Nairobi ilikuwa na nia moja tu; Kuchangisha fedha za kusaidia wagonjwa wa saratani.

Soma hadithi nyingine:

 Kupitia mtandao wake wa Instagram, Gidi ametangaza kuwa atakuwa anasheherekea birthday yake katika miji minne mikuu duniani.