Mwanamke mmoja amekiri kwamba amekuwa akijishughulisha na biashara ya kuwadunga dawa wanawake ili waweze kuafikia mahitaji ya wateja hao wao wa kike . Amesema ‘unapigwa shindano ukiwa ndani ya stall’. Kulingana naye,matibabu hayo bandia na hatari kwa afya hutolewa katika duka zao na hata kuna wahudumu wanaovalia aproni za madaktari ilhali hawajahitimu .
Hata hivyo ametoa ufichuzi ambao utawashangaza wengi wakiwemo waliodungwa sindano za kuongeza kiasi cha sehemu wanazotaka Wamekuwa wakidungwa sindano zenye maji na hata sio kemikali zinazoahidiwa kutumiwa . ‘Kuna wale ambao hata huzirai tukiwadunga, haifanyangi kazi ni maji plain’ amesema .
Kumekuwa na visa vya wanawake na wasichana kukosa kuamini maombo yao na kufedheheshwa kwamba labda hawavutii jambo ambalo limewatia wengi mashakani kwa kujiingiza katika njia hatari za kujaribu kujibadilisha kimuonekano na kuhatarisha maisha yao .