Nikiskia jina Tanasha ,najua ni baby mama asema Willy Paul

NA NICKSON TOSI

Mwanamziki Willy Paul ameibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki katika mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba akiskia jina Tanasha kinachomjia akilini mwake ni kuwa yeye ni Baby mama.

Willy alisema haya akiwa katika mahojiano na stesheni moja ya humu alipoulizwa swali kuhusiana na msanii huyo wa Kenya aliyekuwa na uhusiano na Diamond kabla ya kutengana.

'Mimi nikiskia jina, Tanasha', najua ni baby mama aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond na baadaye wakaachana. Ni hayo tu ninayofahamu kuhusiana na msanii huyo,' alisema willy.

Mimi nimeoa mpenzi wangu wa muda, anatoka taifa la Jamaica na tumeamua kuanzisha familia yetu mimi na yeye baada ya kuchumbiana kwa muda. Alisema Pooze.

Usemi wake kuhusiana na Tanasha aidha uliibua hisia kubwa mtandaoni wengi wakimtaja kama msanii anayependa kuhanya hanya na matendo yake yasioambatana na dini.

Maajuzi willy amekiri atatoa wimbo na chipukizi mtindo wa kufoka nchini maarufu kama gengetone, hatua iliyowafanaya wasanii katika sekta ya miziki ya injili kumsomea kwa kile walisema ni kunajisi nyimbo za kumtukuza Mungu kwa lengo la kujipatia mihela.

Baadhi ya wafwasi wake walisema hayo.

 apo kwa Tanasha 🔥🔥🤣🤣🤣

 🤣🤣🤣huyu ni diamond mdogo

 😂😂 woii ya Ringtone