Baadaye aligundua kwamba mke wake alikuwa na mimba ya mtu mwingine aliyopata hata kabla wawili hao hawajaoana . Ben amesema likutana na mkewe mwaka wa 2008 na wakafanya uchumba kwa mwaka mmoja kabla ya kuoana .Walipima ukimwi ili kujua hali zao lakini mkewe alikataa kupima uja uzito . Ben anasema wakati ho hakuelewa mbona mwenzake alikuwa hataki kupima ili kufahamu iwapo alikuwa na uja uzito .wakati wa harusi anasema alipokuwa akimshika mkono mkewe ,alikuwa akimuachilia na hata hakutaka wapigwe picha pamoja .
‘Sikuelewa mbona hakuwa na furaha’ Ben anasema
Siku ya kwanza ya Fungate yao mkewe alisema alikuwa akiumwa na kichwa na siku ya pili alisema alikuwa akiumwa na tumbo .
‘Kila siku ya wiki ,alikuwa na kisingizio’ anasema Ben .
Fungate yao ilidumu wiki moja na wakati huo wote hawakushiriki tendo la ndoa .Ben anasema alimbembeleza lakini hakufanikiwa . Baadaye mkewe alianza kuwa mjeuri na kutumia lugha ya matusi na hata wakati mwingine kumpiga Ben .
‘Tuliporudi nyumbani ,nilipika na siku ya pili nikafua nguo zetu kwa sababu alisema alikuwa akiugua bado’.
Ben anasema mkewe alianza kumpa masharti mengi na akajipata na ugonjwa wa vidonda vya tumbo .Kitu ambacho hakujua wakati huo ni kwamba ndoa yao ilikuwa imeshatumbukia nyongo . Baada ya mwaka mmoja walipotengana ,Ben aliambiwa na jamaa ya mke wake kwamba alifanya vizuri kumuacha kwa sababu alikuwa mja mzito na mimba ya mtu mwingine . Alipotoka katika nyumba yao alienda ana akaitoa mimba hiyo . Ben aligundua baadaye sababu hiyo ndio iliyomfanya kukata kupima uja uzito .