Kamenuka: Gari ambalo Diamond alimzawidi Tanasha sasa ni la mamake!

dangote
dangote
Tangia Tanasha na Diamond watengane majuma kadhaa yaliyopita, mengi yametendeka, moja ikiwa kuwa Sarah Dangote, ambaye ni mamake msanii huyo kuvinyakua vitu vilivyomilikiwa na Tanasha.

Mama Dangote sasa hivi ndiye mmiliki wa gari la aina ya Prado, gari ambalo Tanasha alizawidiwa na Diamond. Habari na uhondo huu mpya ulitolewa na Juma Lokole ambaye ni rafiki wa karibu wa Diamond Platnumz.

Mengi yamekuwa yakitendeka tangia Tanasha amteme Diamond kwa kile kinaaminika kuwa kutoaminika kwa msanii huyo na akaamua kurudi nchini Kenya.

Uvumi unaoenea ni kwamba gari ambalo Diamond alilomzawidi Tanasha wakati wa sherehe za siku ya kuzaliwa kwake zilizotambulika kama 707TheGreatGatsby ilikuwa ni karata tu.

Diamond aliwazawidi mamake na Tanasha kila mmoja gari lakini ukweli wa mambo ni kuwa magari yote yalikuwa ya mama Dangote.

Juma alifichua kuwa kwa muda huo wote, magari yote yalikuwa yamesajiliwa kwa jina la Mama Dangote huku ikiaminika sherehe hiyo yote ilikuwa tu ya kutafuta kiki.

Uhondo huu ulikuja baada ya shabiki mmoja kumuuliza Juma iwapo Diamond ambaye sasa hivi hana kazi kwa ajili ya virusi vya Corona - iwapo atauzia mamake gari moja.

“THE CAR IS STILL THERE. WHY SHOULD IT BE SOLD? NASEEB IS NOT ONE TO SELL HIS PROPERTY,” ALISEMA.

Alipoulizwa mbona hakubeba gari lake baada ya kumtenga Diamond mwenye tabia ya mipango ya kando, Juma alijibu kuwa gari hilo sio la Tanasha na kuwa lina mmiliki kamili.

“WHY SHOULD TANASHA LEAVE WITH THE CAR? THE CAR BELONGS TO MAMA DANGOTE. IN FACT BOTH THE CARS,” ALISEMA.

Haya hii ni kama ndrama ama 'vindeo' na kila siku uhondo mpya hutokea kuhusu wawili hawa. Kile ambacho tutakuarifu ni kuwa usikae mbali kwani tutakuarifu pindi tutakapopata mapya.