Aliyefanya kitendo hiki hatawahi ona mlango wa Mbinguni,Asema Vera Sidika

NA NICKSON TOSI

Vera Sidika amejikuta katika njia panda baada ya wanannchi kutumia picha zake akiwa nusu uchi kueneza jumbe za kutaka watu wazingatie usafi kama njia ya kukabili virusi Vya Corona.

Alhamisi mwanasosholaiti huyo alituma picha katika mitandao ya kijamii akijiuliza maswali ni kwanini watu waliamua kutumia picha yake  visivyo, anasema picha hiyo ilikuwa imeandikwa onyo kuhusiana na hatari ya kushika usoni kwa mikono chafu.

Kuna hii picha inayozagaa katika mitandao ya kijamii ,aliyefanya hivyo hatawai ona mlango wa kuingia mbinguni kamwe 😂🤣😂 ❤️  🤣”aliandika Vera.

Picha hiyo ilikuwa na maandishi usijishike macho,mapua namdomo kama hujaosha mikono, kaa nyumbani kama uko na dalili zozote za Corona, maandishi hayo yalimfanya Vera kuwa na hamaki kwani anahisi kuwa picha yake ilitumiwa visivyo.

Wakenya walikuwa na haya ya kusema kuhusiana na picha hiyo katika mitandao ya kijamii.

 “Tungetengeneza picha kama za GIG alafu ttuewaambie wananchi wanawe mikono mara hiyo.”

 “🤣🤣🤣🤣”

 “🤣🤣🤣🤣🤣”

 “Chukua io COAT of arms apo upelekee watoto wako nyumbani 😂😂😂”

 “Wacha tunyonge nyani  na hii🙊🙊”

 “Ona sasa umenitobolea boxer@queenveebosset”