Bila kujua kilichokuwa kinaendelea ,Kelvin Maina hakujua mke wake wa zamani alikuwa na njama ya kumuua . Mshukiwa alifaulu kumhadaa hadi katika nyumba yake mtaani Mathare na Kumdunga kisu kifunia mara mbili siku ya jumatatu . Baadaye Mary alikamatwa na maafisa wa DCI na anazuiliwa kwa siku 14 huku uchunguzi kuhusu mauaji ya mume wake wa zamani yakichunguzwa . Corporal Christopher Samoei wa DCI pangani aliongoza uchunguzi uliopelekea kukamatwa kwa Mary pamojana kupatikana kwa silaha iliyotumiwa kwa mauaji ya mume wake wa zamani katika nyumba yake .
Mshukiwa alikamatwa katika eneo la Muthaiga-Kosovo Machi tarehe 16 na uchunguzi dhidi yake unaendelea.Samoei amesema kisu kilichotumiwa kumuua Kelvin kilipatikana na mabki ya damu na kimepelekwa kwa mwanakemia wa serikali kwa uchunguzi zaidi .
Polisi wamesema wanahitaji kuzichukua simu za mshukiwa na mumewe kwa uchunguzi wa kubaini jumbe walizokuwa wamebadilishana kabla ya Kelvin kwenda katika nyumba ya mke wake wa zamani alikouawa .